Ephesians 1

Salamu

1 aPaulo, mtume wa Al-Masihi Isa, kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu:

Kwa watakatifu walioko Efeso, walio waaminifu katika Al-Masihi Isa:

2 bNeema na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana wetu Isa Al-Masihi iwe nanyi.

Baraka Za Kiroho Katika Al-Masihi Isa

3 cAhimidiwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Isa Al-Masihi, aliyetubariki sisi kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho ndani ya Al-Masihi. 4 dKwa maana alituchagua katika yeye kabla ya kuumbwa ulimwengu ili tuwe watakatifu na bila lawama mbele zake. Kwa upendo 5 ealitangulia kutuchagua tuwe wanawe kwa njia ya Isa Al-Masihi kwa furaha yake na mapenzi yake mwenyewe. 6 fKwa hiyo tunamsifu Mungu kwa huruma zake kuu alizotumiminia sisi katika Mwanawe Mpendwa. 7 gNdani yake tunao ukombozi kwa njia ya damu yake, yaani, msamaha wa dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake 8 haliyotumiminia kwa wingi, kwa hekima yote na maarifa yote. 9 iNaye alitujulisha siri ya mapenzi yake sawasawa na uradhi wa mapenzi yake, ambayo alikusudia katika Al-Masihi, 10 jili yapate kutimizwa wakati mkamilifu utakapowadia, yaani, kuvitia vitu vyote vya mbinguni na vya duniani pamoja, chini ya kiongozi mmoja, ndiye Al-Masihi.

11 kKatika Al-Masihi sisi nasi tumepata urithi, tukisha kuchaguliwa sawasawa na kusudi la Mungu, yeye ambaye hufanya mambo yote kulingana na kusudi la mapenzi yake, 12 lili kwamba, sisi tuliokuwa wa kwanza kuweka tumaini katika Al-Masihi, tupate kuishi kwa sifa ya utukufu wake. 13 mNinyi pia mliingia ndani ya Al-Masihi mliposikia Neno la kweli, Injili ya wokovu wenu. Mkiisha kuamini, ndani yake mlitiwa muhuri, yaani, Roho Mtakatifu mliyeahidiwa, 14 nyeye ambaye ni amana yetu akituhakikishia urithi wetu hadi ukombozi wa wale walio milki ya Mungu kwa sifa ya utukufu wake.

Shukrani Na Maombi

15 oKwa sababu hii, tangu niliposikia juu ya imani yenu katika Bwana Isa na upendo wenu kwa watakatifu wote, 16 psijaacha kumshukuru Mungu kwa ajili yenu, nikiwakumbuka katika maombi yangu. 17 qNazidi kumwomba Mungu wa Bwana wetu Isa Al-Masihi, Baba wa utukufu, awajalieni ninyi roho ya hekima na ya ufunuo, ili mpate kumjua zaidi. 18 rNinaomba pia kwamba macho ya mioyo yenu yatiwe nuru ili mpate kujua tumaini mliloitiwa, utajiri wa urithi wa utukufu wake kwa watakatifu 19 sna uweza wake mkuu usiolinganishwa kwa ajili yetu sisi tuaminio. Uweza huo unaofanya kazi ndani yetu, ni sawa na ile nguvu kuu mno 20 taliyoitumia katika Al-Masihi alipomfufua kutoka kwa wafu, na akamketisha mkono wake wa kuume huko mbinguni, 21 ujuu sana kuliko falme zote na mamlaka, enzi na milki, na juu ya kila jina litajwalo, si katika ulimwengu huu tu, bali katika ule ujao pia. 22 vNaye Mungu ameweka vitu vyote viwe chini ya miguu yake na amemfanya yeye awe kichwa cha vitu vyote kwa ajili ya Kanisa, 23ambalo ndilo mwili wake, ukamilifu wake yeye aliye yote katika yote.
Copyright information for SwhKC